Arafat Ally Haji (@arafat__ah) 's Twitter Profile
Arafat Ally Haji

@arafat__ah

Father||CEO @pbzbank ||Vice President @YoungAfricansSC ||Board Member @wrrbtz|| ACI FMA Certified||Views Expressed here are my own,#NasahaZaAAH,RT~ Read This ||

ID: 192613632

linkhttp://www.pbzbank.co.tz calendar_today19-09-2010 17:24:35

65,65K Tweet

78,78K Followers

1,1K Following

Arafat Ally Haji (@arafat__ah) 's Twitter Profile Photo

#NasahaZaAAH “Leo jua litawaka sana, kesho mvua itanyesha sana, jana kiza kilitanda sana ila leo pamekucha na kupambazuka, ni kama maisha yalivyo utapitia changamoto na utapitia ushindi, utapitia dhiki na utapitia faraja, Mshindi kati yetu ni yule aliyeshikilia kamba ya

Arafat Ally Haji (@arafat__ah) 's Twitter Profile Photo

#NasahaZaAAH “Hakuna chochote ambacho Mwenyezi Mungu ametuahidi hapa duniani isipokuwa KIFO, ukilifahamu hilo basi tambua mali zina mwisho, majivuno yana mwisho, Utajiri una mwisho na kinachosalia ni maisha mema, roho njema na Binadamu wema”

#NasahaZaAAH

“Hakuna chochote ambacho Mwenyezi Mungu ametuahidi hapa duniani isipokuwa KIFO, ukilifahamu hilo basi tambua mali zina mwisho, majivuno yana mwisho, Utajiri una mwisho na kinachosalia ni maisha mema, roho njema na Binadamu wema”
Arafat Ally Haji (@arafat__ah) 's Twitter Profile Photo

#NasahaZaAAH “Unapofeli usiwazuie kukucheka, unapofaulu usilazimishe wakusifie, huhitaji kelele zao wala pongezi zao, unahitaji macho na masikio yao washuhudie namna unafanya vitu vitokee”

Arafat Ally Haji (@arafat__ah) 's Twitter Profile Photo

#NasahaZaAAH “Wanaweza wasithamini uwepo wako, wasitambue kazi yako, hakikisha unaishi na kutengeza alama yako, acha wasitambue thamani yako ila watambue kukosekana kwako kuna athari, Ishi kama CHUMVI, ikiwepo haithaminiwi, ikikosekana Chakula hukosa ladha.”

Arafat Ally Haji (@arafat__ah) 's Twitter Profile Photo

#NasahaZaAAH “Tukiumizwa tunapaswa kulia lakini tukisonga mbele, tunapofeli tunapaswa kujipanga, tunapokosewa tunapaswa kusamehe, tunapooneshwa dharau sisi tuwalipe heshima, hatulipi ubaya kwa ubaya, hatuiti kisu kwa kisu, tunalipa upendo kwenye chuki, tunalipa wema kwenye

Arafat Ally Haji (@arafat__ah) 's Twitter Profile Photo

#NasahaZaAAH “Kuwa makini wakati unashinda ila kuwa makini zaidi wakati unaanguka, ushindi una Watu na shangwe ila anguko lina majuto na dharau, zote ni baraka za Mungu kwa namna tofauti zipokee vyema”

Arafat Ally Haji (@arafat__ah) 's Twitter Profile Photo

#NasahaZaAAH “Tuna makosa yetu ila tuna mema yetu, tuna uzuri wetu na tuna ubaya wetu, tuna vilio na furaha kwenye maisha yetu na maisha ya wengine, akitokea Mtu akahubiri mabaya yetu kuliko mazuri yetu basi hatutajielezea kwakuwa Binadamu hutaka kusikia anachotaka kuambiwa”

Arafat Ally Haji (@arafat__ah) 's Twitter Profile Photo

#NasahaZaAAH “Usisahau kuna wakati wakishakuumiza watarudi kuulizia unaendeleaje ili wapime ukubwa wa majeraha waliyokuachia, waache waende tutawapa tabasamu, wakirudi tutawaonesha tabasamu, ushindi wao ni kutuona tukiumia na wanaumia sana kuona hatujaumia”

Arafat Ally Haji (@arafat__ah) 's Twitter Profile Photo

#NasahaZaAAH “Ndege akikaa kwenye Mti mmoja kwa muda mrefu basi huyo anataka kupigwa jiwe, haijalishi pana uzuri kiasi gani, haijalishi unapapenda kwa namna gani, ukikaa hapo kwa muda mrefu unaalika Maadui”

Arafat Ally Haji (@arafat__ah) 's Twitter Profile Photo

#NasahaZaAAH “Wanaweza kukutendea ubaya ukaridhika na kumshukuru Mungu, ukaamua kuishi maisha yako na bado wakaumia kisa kufurahia shida zako, Binadamu hao”

Arafat Ally Haji (@arafat__ah) 's Twitter Profile Photo

#NasahaZaAAH “Penda sana kutumia neno TUMEFANYA, husudu neno TUMESHINDA, usikimbilie kusema neno TUMEPOTEZA kama hujawahi kusema TUMEFANYA, popote tanguliza wingi, jiweke nyuma ama kaeni mbele nyote kwa pamoja, mwisho wa siku mtafanya kwa wakati wenu na kuondoka zenu”

Arafat Ally Haji (@arafat__ah) 's Twitter Profile Photo

#NasahaZaAAH “Kwenye mapambano upo kwenye chumba cha peke yako ambacho ni kidogo kama Kaburi, ila utakapofanikiwa watu watajaza ukumbi kukupigia makofi, uhalisia ni kuwa hakuna anayejali shida zako ila ukishinda tutazipenda hela zako, ukifahamu hilo umeyafahamu maisha”

Arafat Ally Haji (@arafat__ah) 's Twitter Profile Photo

#NasahaZaAAH “Ukiwa unamenya karanga za Kipofu, hakikisha unapiga sana miruzi ili awe na amani kuwa hauli karanga zake, kwenye kila kazi ya watu utakayopewa basi jitahidi sana kuwa muumini wa kurejesha taarifa kila wakati”

Arafat Ally Haji (@arafat__ah) 's Twitter Profile Photo

#NasahaZaAAH “Usiwakadirie sana Watu, usidharau Watu, usichukulie poa Watu, wenzako wanapambana kubadili historia ya maisha yao na kushinda vita ambazo Wazazi wao hawakuzishinda, wao ndio wana dhamana ya kubadili historia ya familia zao, kama huwezi kuwasaidia tafadhali usinunue

Arafat Ally Haji (@arafat__ah) 's Twitter Profile Photo

#NasahaZaAAH “Sio kila mmoja ataelewa ugumu au maana ya safari yako ya maisha na hilo ni sawa tu, kwakuwa wanapaswa kuielewa zaidi safari yao na sio safari yako, bila kujali wanasema nini wewe endelea kusonga kwakuwa ni safari yako sio yao, ni desturi ya Washindi kuwaza mambo