Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile
Dazzy Elly

@asajiledaniel

Hustling is my favorite game.

ID: 1735920131639836672

calendar_today16-12-2023 07:10:22

185,185K Tweet

5,5K Followers

7,7K Following

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Mpaka pale tutakapoacha uoga wa mabadiliko ndio tutakapopata viongozi sahihi ambao watakua ndio wanaogopa kutudanganya na kutuona hatuna akili. Sisi ndio waajiri wa viongozi na tunatakiwa tuwe na nguvu juu yao,uoga wetu unatutesa siku zote. We need to change. Blessed weekend.

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Katika kuomba kwa Mungu, tunatakiwa kushukuru kwa tulivyo navyo kwanza na kuomba ulinzi juu yake na ndio inakuja kuomba vile tunavyo tamani kuwa navyo. Kumbuka pia kuwa Mungu anakupa vile unavyo stahili. May we have a blessed sunday and get what we deserve. Good morning fam.

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Ni ngumu sana kupendwa kwa muonekano wa nje tu kama muonekano wako wa ndani ni mchafu,zaidi utaishia kutumika na kutupwa na kila akupatae. Ubora wa mtu haupimwi na muonekano wake wa nje bali wa ndani zaidi yani vile vitu visivyopoteza mvuto wala kuzeeka. Good morning fam.

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Usiishi kwa kufuata mkumbo,macho na akili unavyo.Vitumie vyema. Angalia jamii uliyopo kisha tafakari,kati ya wewe na jamii yako je kipi kinahitaji mabadiliko? Jibu lako lifanyie kazi,kila kitu huanza ndani ya akili ya mtu mmoja tu.Jukumu letu kuleta maendeleo. Good morning fam.

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Ile kauli ya "Kua uyaone" ni kama huwa inabeba laana fulani maana ukishakua unaona kila rangi mpaka unaanza kujiuliza ndio haya niliyokua naambiwa niyaone,ukiwa mdogo unakua huwezi elewa maumivu wanayopitia watu wazima na unaona ni kawaida tu. Sio rahisi kuwa mkubwa. Gm fam.

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Ndoa na mahusiano mengi vimekua ni killing agents. Watu wanapitia maumivu makali mno ambayo yanawaua taratibu kila siku zinapoenda. Kuishi na binadamu mwenye mapungufu kiasilia ni ngumu mno. Ukiuliza wengi walio kwenye ndoa wanaweza kukuambia bora wasingeingia. Good morning fam.

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Ukipata mtu anayeweza kushirikiana nawe kutatua tatizo ulilonalo basi jitahidi umshikilie kwa nguvu zote,huo ni upendo halisi,alikua na chaguo jepesi la kutafuta kilicho bora. Ubaya ni kuwa siku hizi msaada pekee unaothaminiwa ni pesa tu,tumesahau utu. Good morning fam.

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Hivi kazi ya wahariri kwenye vyombo vya habari ilibadilika? Kiongozi anaweza kuongea uongo wa wazi kabisa na takwimu zipo wazi za kumkanusha lakini unakuta chombo cha habari kimetoa habari kama ilivyo - Uchawa ni mbaya sana. Imekua kero kuangalia na kusoma habari sasa. Good day.

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Kuwa mwanaume tajiri nayo ni tabu sana,ile kauli ya "je ukifa mapema itakuaje?" Inakua ni maombi ya wewe kufa mapema. Kuanzia ndugu zako,mkeo,watoto na vijakazi wako,wote wanakua wanawaza ukidondoka itakuaje? Ni ngumu sana kuwaziwa kwa upendo pesa ilipotawala. Good morning fam.

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Mtoto wa kiume huwa anasisitizwa aoe ili apate motisha ya kutafuta maisha kwa bidii,wazazi huwa wanaamini akiwa ana majukumu na wajibu wa kutimiza basi hawezi kubweteka. Mtoto wa kike atakumbushwa kuolewa umri unavyosogea tu. Blessed sunday and a very good morning my friends.

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Dini tofauti ila Mungu ni mmoja,kuna vitu viko wazi sana yani sio mtazamo wala tafsiri ya kitabu cha Mungu. Kwanini hawa viongozi wa dini watofautiane? Serikali imesaliti wananchi na dini imesaliti waumini. Tunahubiri amani kwenye Giza,taifa linapoteza muelekeo kila siku. Gm fam

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Wanasema kula raha maisha ni mafupi,ni kweli maisha ni mafupi ila ukiyapa lengo huwa ni marefu na ya kuridhisha.Uelekeo ndio kila kitu. Wengi waliowekeza kwenye kula raha waliyafupisha maisha yao,starehe zina mtindo wa kufanya ulipie madhara yake muda mfupi tu. Good morning fam.

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Njia ya uhakika ya mwanaume kuchelewa kimaendeleo au kurudi nyuma ni kuwa na mwanamke masikini mwenye high standards. Mapenzi ni sumu kwa mwanaume anayejitafuta,wengi wamefeli mazima kisa walitumikia vitu viwili kinzani kwa wakati mmoja. Kaa kwenye mstari. Good morning fam.

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Watu wengi huwa wanahakiki ubora wao au umependo kutoka kwa watu wengine.Huo ni utumwa wa kifikra na kihisia,kitu bora ni bora tu hata kisiposifiwa wala kuongelewa na hutajali upendo wa mtu mwingine kama unajipenda mwenyewe zaidi. You are who you are,no need for approval. Gm fam

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Ukiacha lalama unapofeli katika mapambano unaweza kuona maana nzuri ya kufeli,ukiachana na kujifunza kuna uwezekano mkubwa sana mlango uliofungwa ni safari ya kuelekea kwenye mlango sahihi,wengi imetutokea hii unasema bora nilikataliwa pale,sasa nipo pazuri. Good morning fam.

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Adui hodari ni muhim kuliko rafiki bora,watu huhitaji nguvu ya msukumo ili kujinoa na kuwa bora zaidi,huyo adui hodari atakunyima usingizi utakua unawaza kila muda jinsi ya kujiimarisha kuwa bora zaidi yake. Sio ule uadui wa kurogana.Bila Samsung,iPhone sio kitu Good morning fam

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Tunajifunza kutokana na makosa ila sio lazima ufanye wewe makosa yote ndio ujifunze,tumia zaidi makosa ya jirani kujifunza,utakua umepunguza makovu mwilini mwako.Ndio ile kauli ya kusema unashtakiwa kwa kosa hili na adhabu hii ili wengine wajifunze kupitia wewe. Good morning fam

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Nothing is perfect. Ukipenda mtu mzuri sana pia ue tayari kuishi na lile pungufu lake kuu,fuatilia kwa ukaribu utaona ukweli, mzuri zaidi ndio ana tatizo kubwa zaidi. Mungu aliamua kuweka mzani ili tusidharauliane sana,ukileta dharau ni kiburi chako tu. Good morning fam.

Dazzy Elly (@asajiledaniel) 's Twitter Profile Photo

Wanaume huwa wanaenda kwa reasoning ila wanawake hutumia hisia,inapelekea wachungaji wengi sana kukimbilia kwa wanawake. Nenda kanisa lolote chukua takwimu utaona. Imeibuka hatari mpya,wachungaji wa kileo wapo tayari wavunje ndoa ili wapate muumini. Ni Mungu au ushetani? Gm fam.