Dr Hussein Ali Mwinyi (@drhmwinyi) 's Twitter Profile
Dr Hussein Ali Mwinyi

@drhmwinyi

A Proud husband and a Father | President of The Revolutionary Government of Zanzibar

ID: 1282980411417726981

linkhttp://www.husseinmwinyi.co.tz calendar_today14-07-2020 10:09:30

499 Tweet

199,199K Followers

7 Following

Dr Hussein Ali Mwinyi (@drhmwinyi) 's Twitter Profile Photo

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Donge, Mkuu wa Mkoa wa Kusini, Pemba Mhe. Pembe Juma Khamis kilichotokea leo: 06. Machi 2023   Nawatakia moyo wa subira Wanafamilia, Ndugu, Jamaa na Marafiki kipindi hiki kigumu cha msiba.   Amin

Dr Hussein Ali Mwinyi (@drhmwinyi) 's Twitter Profile Photo

Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya kifo cha Ndugu Benard Membe ambaye alikuwa kiongozi mwenye uwezo mkubwa, mwanadiplomasia,na mtumishi shupavu wa taifa Natoa pole kwa familia, marafiki na wote walioguswa na msiba huu Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani. Amin

Dr Hussein Ali Mwinyi (@drhmwinyi) 's Twitter Profile Photo

Nachukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Dr Salim Ahmed Salim kwa kutunukiwa Tuzo ya Heshima iitwayo Order of Amilcar Cabral, First Degree na Rais wa Cape Verde Mhe. Dkt. Jose Maria Neves kwa mchango wake mkubwa katika ukombozi wa Bara la Afrika.

Nampongeza Mhashamu Baba Askofu Mkuu Mwandamizi Protase Rugambwa kwa kuteuliwa na Baba Mtakatifu Fransisko kuwa Kardinali wa Tatu wa Tanzania. Naungana na Watanzania kukutakia heri kwa majukumu yako mapya katika Kanisa Katoliki nchini. Mwenyezi Mungu aendelee kukusimamia.

Nampongeza Mhashamu Baba Askofu  Mkuu Mwandamizi Protase Rugambwa kwa kuteuliwa na Baba Mtakatifu Fransisko  kuwa  Kardinali  wa Tatu wa Tanzania.

Naungana na Watanzania kukutakia heri kwa majukumu yako mapya katika Kanisa Katoliki nchini.

Mwenyezi Mungu aendelee kukusimamia.
Dr Hussein Ali Mwinyi (@drhmwinyi) 's Twitter Profile Photo

Nimepokea kwa huzuni taarifa ya kifo cha Shafii Abubakar mtoto wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir kilichotokea jana: 28 Agosti 2023, Dar es Salaam Allah awape nguvu na subira familia, ndugu na marafiki kipindi hiki cha msiba Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un

Dr Hussein Ali Mwinyi (@drhmwinyi) 's Twitter Profile Photo

On behalf of the people of Zanzibar,my heartfelt condolences to King Mohammed VI,the bereaved families,and Moroccans during this difficult time. My sincere respect for the many individuals who are providing emergency support and rescue efforts. You are in our thoughts and prayers

Dr Hussein Ali Mwinyi (@drhmwinyi) 's Twitter Profile Photo

Nachukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU Kuchaguliwa kwako kunatokana na jitihada zako ambazo zimejengwa na uchapakazi, uzoefu, uaminifu na uadilifu pia kuiongezea heshima nchi yetu.

Dr Hussein Ali Mwinyi (@drhmwinyi) 's Twitter Profile Photo

Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Issa Juma Nangalapa kaka yake Waziri Mkuu Mhe. Kassim M. Majaliwa kilichotokea jana tarehe: 05 Nov, Dar es Salaam. Allah awape nguvu na subira familia, ndugu na marafiki kipindi chote cha majonzi. Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un

Dr Hussein Ali Mwinyi (@drhmwinyi) 's Twitter Profile Photo

Namshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema kwa kufikisha miaka 57 leo. Kwa furaha pia nawashukuru wote mlioikumbuka siku yangu ya kuzaliwa, Asanteni kwa upendo na jumbe zenu za heri, Mwenyezi Mungu awabariki nyote.

Dr Hussein Ali Mwinyi (@drhmwinyi) 's Twitter Profile Photo

Nimezindua rasmi Jezi ya timu ya Taifa ZANZIBAR HEROES katika viwanja vya Nyamanzi Mjini Magharibi, Unguja tarehe: 26 Januari 2024. Jezi mpya za ZANZIBAR HEROES zitatumika katika mashindano ya madaraja mbalimbali ya uwakilishi ndani na nje ya nchi.

Dr Hussein Ali Mwinyi (@drhmwinyi) 's Twitter Profile Photo

Happy Chinese New Year! Let's celebrate the growing diplomatic relations between China and Zanzibar, fostering trade, investment and development cooperation. May the Year of the Dragon bring abundant joy, laughter and prosperity to all. #YearOfTheDragon #ChineseNewYear2024

Dr Hussein Ali Mwinyi (@drhmwinyi) 's Twitter Profile Photo

Leo ni Jumatano ya Majivu na mwanzo wa siku 40 za Kwaresima. Katika kipindi hiki cha toba na matumaini mapya kiroho, tujitafakari na kuiombea nchi yetu amani na mshikamano katika sala na mfungo. Nawatakia Wakristo wote baraka tele na mfungo mwema.

Dr Hussein Ali Mwinyi (@drhmwinyi) 's Twitter Profile Photo

Nawatakia Krismasi njema yenye upendo, umoja, na maadili kwa familia na jamii kwa ujumla katika msimu huu wa sikukuu. Ni jukumu letu kuendelea kukumbushana umuhimu wa kuimarisha udugu, amani, utulivu, na mshikamano baina yetu. Heri ya Krismasi, mapumziko mema, na baraka tele.

Dr Hussein Ali Mwinyi (@drhmwinyi) 's Twitter Profile Photo

Leo ni Jumatano ya Majivu, mwanzo wa siku 40 za Kwaresima. Hiki ni kipindi cha toba, unyenyekevu kupitia sala na mfungo. Tuombee amani na mshikamano wa nchi yetu, tukimwomba Mwenyezi Mungu atuongoze katika safari hii ya kiroho. Nawatakia Wakristo wote baraka tele na mfungo mwema