
#ElimikaWikiendi
@elimikawikiendi
#ElimikaWikiendi empowers youth through education. We provide platforms for youth to connect, learn and address key challenges that limit their potential
ID: 701453045880717312
21-02-2016 17:06:53
146,146K Tweet
80,80K Followers
500 Following






“Baba ndani ya familia ni walinzi wanapopata elimu ya hedhi huwa msaada kupata vifaa vya kujisitiri na mazingira kuboresha mazingira salama.” allenkaiza_ #ElimikaWikiendi


“Hedhi salama ni yale mazingira sahihi na salama kwa binti na mwanamke kupata sehemu nzuri yenye huduma ya taulo za kike, maji na mahala pa kuhifadhia.” Jennifer Kayombo🌙🕋 #ElimikaWikiendi


“Baadhi ya jamii kwa kuona aibu kipindi cha hedhi wasichana hutumia vifaa ambavyo vinaathiri afya zao za uzazi hili huwaathiri kupata maambukizi.” - Jennifer Kayombo🌙🕋 #ElimikaWikiendi



“Kwa sasa mfumo wa elimu unatoa nafasi ya kutosha kwa wanafunzi kujifunza kuhusiana na hedhi kutokana na mfumo wa pamoja kuhusu Afya ya Uzazi.” Eng. Aysha mkurugenzi Glaring Future Foundation #ElimikaWikiendi


“Umasikini ni kikwazo kinachopelekea wazazi husasani kuamua vipaumbele kati ya kutoa hela ya chakula au kuwapa mabinti fedha ya kununua taulo za kike.” - Jennifer Kayombo🌙🕋 #ElimikaWikiendi


“Gharama za taulo za kike bado ni changamoto kubwa ya kufikia Usawa wa Kijinsia hususani mtoto wa kike kuweza kusoma na kumaliza elimu.” - Monica Patrick #ElimikaWikiendi


“Kupelekea taulo za kike shuleni si kutatua changamoto ya ukosefu wa pedi ni muhimu sasa wazazi kuchukua jukumu hili msingi.” - allenkaiza_ #ElimikaWikiendi


“Binti anapaswa kupatiwa elimu ya hedhi ili aweze kujiandaa na kufahamu ni hali ya kawaida.” - Jennifer Kayombo🌙🕋 #ElimikaWikiendi


“Serikali kupitia wizara ya elimu huwa inatenga bajeti ya taulo za kike shuleni na zinasambazwa ila inahitajika bajeti ya kutosha zaidi.” - allenkaiza_ #ElimikaWikiendi


From joining #ElimikaWikiendi as a regular user of the #ElimikaWikiendi hashtag to now leading as Executive Director. What started as an online learning space is now a movement driving real change. I am honored to lead this next chapter, where young voices shape the future.


