NemcTanzania (@nemctanzania) 's Twitter Profile
NemcTanzania

@nemctanzania

Karibu katika Ukurasa Rasmi wa wa Twitter wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)

ID: 918056846212108288

linkhttps://www.nemc.or.tz/ calendar_today11-10-2017 10:13:03

2,2K Tweet

1,1K Followers

128 Following

NemcTanzania (@nemctanzania) 's Twitter Profile Photo

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt.Immaculate Sware Semesi amebainisha kuwa matumizi ya plastiki yameendelea kuwa chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira, yakiwa na madhara kwa afya ya binadamu na ikolojia ya ardhi

NEMC imeshiriki kongamano la kuhitimisha programu ya mafunzo (ITP 308) kuhusu udhibiti wa maji taka na taka zitokanazo na shughuli za uchimbaji wa madini, nchini Sweden kuanzia tarehe 19-27 Mei, 2025. Kongamano hilo liliandaliwa na Shirika la Utafiti wa Madini la Sweden (SGU).

Mratibu wa Kitaifa wa Mfuko wa Kimataifa wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi (Adaptation Fund) Bw. Fredrick Mulinda ametoa Mafunzo kwa Menejimenti ya NEMC kuhusu kazi, taratibu na mchakato wa kupata na kusimamia fedha za Mfuko wa Kimataifa wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi

Mkurugenzi Mkuu NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi Mei 27,2025 amekutana na kufanya mazungumzo na wajumbe kutoka Jumuiya ya Maridhiano na Amani (JMAT) Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kupokea taarifa fupi la kazi zilizofanywa na JMAT kwenye masuala ya Utunzaji wa Mazingira

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi, Mei 27, 2025 ameongoza kikao cha majadiliano kati ya watumishi wa NEMC na ujumbe kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Sekta ya Nishati na Petroli ya Kenya (EPRA)

NEMC yashiriki kongamano la wakaguzi wa ndani wa Africa lililofanyika Kigali Rwanda tarehe 26/05/ 2025 - 30/05/2025 lenye makusudi ya kuwafunza Wakaguzi wa ndani uongozi bora na mbinu za kusaidia kazi wanazofanya kuleta tija kwenye utendaji kazi wa Taasisi za umma

Tanzania imekabidhi ngao ya Shukrani kwa Shirika la Utafiti wa Madini la Sweden (SGU) ikiwa ni Shukrani kwa Shirika hilo kwa mchango wao mkubwa wa kuwajengea uwezo Maafisa 58 kutoka Tanzania kuhusu udhibiti wa maji na taka zitokanazo na shughuli za uchimbaji wa madini

NEMC Kanda ya Morogori Rufiji yatoa elimu ya Mazingira kuelekea maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani yenye kaulimbiu isemayo *_"Mazingira yetu na Tanzania ijayo, Tuwajibike sasa, dhibiti matumizi ya Plastiki_* "

Meneja NEMC Kanda ya Kaskazini Mashariki Bi. Groly Kombe kwa kushirikiana na maafisa wa Kanda hiyo, Leo tarehe 30 Mei, 2025 ameongoza semina ya utoaji elimu kuhusu usimamizi wa taka za plastiki kwa kuzingatia dhana ya Punguza, Tumia Tena, na Rejeleza.

Meneja NEMC Kanda ya Kaskazini Mashariki Bi. Groly Kombe kwa kushirikiana na maafisa wa Kanda hiyo, Leo tarehe 30 Mei, 2025 ameongoza semina ya utoaji elimu kuhusu usimamizi wa taka za plastiki kwa kuzingatia dhana ya Punguza, Tumia Tena, na Rejeleza

NEMC kwa kushirikiana na Jiji la Dar es salaam kuelekea kilele cha wiki ya mazingira chenye kaulimbiu isemayo "Mazingira yetu na Tanzania ijayo, Tuwajibike sasa, dhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki," wasafisha eneo la kivukoni.

NEMC Kanda ya Bagamoyo wameshiriki Usafi wa Mazingira na upandaji miti uliyofanyika tarehe 31 Mei 2025, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani itakayoadhimishwa tarehe 5 Juni 2025.

Kuelekea Siku ya Mazingira Duniani Juni 5, 2025, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limehimiza wananchi kudhibiti matumizi ya plastiki kwa kupunguza, kutumia tena na kurejeleza kuwa bidhaa nyingine ili kuchochea uchumi rejelezi.