Radio Kaya (@radiokaya) 's Twitter Profile
Radio Kaya

@radiokaya

93.1FmMsa^Kwl ||94.9FmKlf^Voi^LungaLunga|| 99.7FmMlnd^Lamu || - Coast of Kenya (Mombasa)

ID: 84091571

linkhttp://www.radiokaya.co.ke calendar_today21-10-2009 14:30:44

14,14K Tweet

3,3K Followers

847 Following

Radio Kaya (@radiokaya) 's Twitter Profile Photo

Wakazi wa kaunti ya Kilifi wamehimizwa kuhudhuria vikao vya kutoa maoni vinavyopelekwa mashinani ili kuhakikisha wanajihusisha katika uundaji wa sheria na pia kuwawezesha kupata taarifa sahihi kuhusu utendakazi wa serikali. #MulikoLaKaya

Radio Kaya (@radiokaya) 's Twitter Profile Photo

Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka amemkashifu Rais William Ruto kwa kuegemea upande mmoja katika uteuzi wa mwenyekiti na wanachama wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC). #MulikoLaKaya

European Union In Kenya (@euinkenya) 's Twitter Profile Photo

IMPORTANT UPDATE The Opening Ceremony of the EU-Kenya Business Forum 2025 will now begin at 8:00 AM, one hour earlier than previously scheduled.

IMPORTANT UPDATE
The Opening Ceremony of the EU-Kenya Business Forum 2025 will now begin at 8:00 AM, one hour earlier than previously scheduled.
Radio Kaya (@radiokaya) 's Twitter Profile Photo

Shirika la huduma kwa wanyamapori nchini KWS tawi la Watamu kaunti ya kilifi limewaonya wananchi hasa wavuvi dhidi ya kuvua samaki aina ya kasa baharini #MulikoLaKaya

Radio Kaya (@radiokaya) 's Twitter Profile Photo

Wakaazi wa eneo la Ndatani na Tsangatsini wadi ya kayafungo eneo bunge la kaloleni kauti ya kilifi wanaishi kwa hofu baada ya Ndovu kuvamia makaazi yao. #MulikoLaKaya

Radio Kaya (@radiokaya) 's Twitter Profile Photo

Mamlaka ya Kitaifa ya Usalama wa chakula (NBA) imepanga msururu wa ushirikiano na serikali za Kaunti Nchini huku ikilenga kuimarisha elimu kwa umma na kukabiliana na taarifa potofu zilizoenea kuhusu viumbe vilivyobadilishwa vinasaba (GMOs) #MulikoLaKaya

Radio Kaya (@radiokaya) 's Twitter Profile Photo

Rais William Ruto amelihakikishia taifa kwamba wakenya wote waliopotea katika njia tatanishi wameunganishwa na familia zao, akisema serikali yake imeweka mikakati kumaliza visa vya watu kupotea katika hali tatanishi. #MulikoLaKaya

Radio Kaya (@radiokaya) 's Twitter Profile Photo

Waziri wa afya nchini Aden Duale amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka shirika la umoja wa mataifa la kupambana na Ukimwi UNAIDS, ili kujadili mbinu za kuboresha makabiliano dhidi ya virusi vya Ukimwi humu nchini Kenya. #MulikoLaKaya

Radio Kaya (@radiokaya) 's Twitter Profile Photo

Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua anatarajiwa kuongoza hafla ya uzinduzi wa chama cha The Democracy for the Citizens Party inayofanyika Lavington, jijini Nairobi. #MulikoLaKaya

Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua anatarajiwa kuongoza hafla ya uzinduzi wa chama cha The Democracy for the Citizens Party inayofanyika Lavington, jijini Nairobi.
#MulikoLaKaya
Radio Kaya (@radiokaya) 's Twitter Profile Photo

Mtetezi wa haki za binadamu kutoka Uganda Agather Atuhaire, ambaye alikamatwa nchini Tanzania ameripotiwa kuachiliwa #MulikoLaKaya

Mtetezi wa haki za binadamu kutoka Uganda Agather Atuhaire, ambaye alikamatwa nchini Tanzania ameripotiwa kuachiliwa #MulikoLaKaya
Radio Kaya (@radiokaya) 's Twitter Profile Photo

Zaidi ya maskwota elfu 10 katika eneo la Jilore kaunti ya Kilifi wamepata matumaini baada ya serikali ya kuanti ya Kilifi kuanza zoezi la kupima mashamba yao ya takriban ekari elfu 1,500 ili kupewa hatimiliki.#MulikoLaKaya

Radio Kaya (@radiokaya) 's Twitter Profile Photo

Waziri wa Leba nchini Alfred Mutua ameagiza kutiwa nguvuni kwa vijana walioghushi stakabadhi na kujitokeza hapo jana katika kaunti ya Mombasa katika zoezi la kusajili wakenya katika ajira za Ugaibuni. #MulikoLaKaya

Radio Kaya (@radiokaya) 's Twitter Profile Photo

Mchakato wa kuunda tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imekabiliwa na vikwazo vya kisheria, hii ni baada ya mahakama kuu hii leo kuzuia kuchapishwa katika gazeti rasmi la serikali makamishna wapya wa IEBC walioteuliwa. #MulikoLaKaya

Radio Kaya (@radiokaya) 's Twitter Profile Photo

Mjadala kuhusu ubaguzi wa ajira katika bandari ya Mombasa umechacha huku Wakereketwa wa maswala ya kijamii na wale wa kisiasa Kaunti ya Mombasa wakishikilia kwamba ajira hizo zimekuwa zikitolewa kiubaguzi. #MulikoLaKaya

Radio Kaya (@radiokaya) 's Twitter Profile Photo

Bunge la kaunti ya Kilifi limetilia shaka hali ya vijana wa kaunti hiyo kujitenga na vikao vya umma vinavyolenga kujadili maswala mbalimbali yanayofungamana na maendeleo ya kaunti hiyo. #MulikoLaKaya

Radio Kaya (@radiokaya) 's Twitter Profile Photo

Naibu Inspekta jenerali wa Polisi nchini Eliud Lagat ajiondoa katika wadhfa wake kwa muda kupisha uchunguzi wa kifo cha Mwanablogu Albert Ojwang aliyefariki katika mikono ya Polisi. #MulikoLaKaya

Naibu Inspekta jenerali wa Polisi nchini Eliud Lagat ajiondoa katika wadhfa wake kwa muda kupisha uchunguzi wa kifo cha Mwanablogu Albert Ojwang aliyefariki katika mikono ya Polisi.

#MulikoLaKaya
Radio Kaya (@radiokaya) 's Twitter Profile Photo

Bunge la kitaifa limepitisha mswada wa fedha wa mwaka 2025, baada ya kuondoa pendekezo la kuipa uwezo mamlaka ya ukusanyaji ushuru KRA kupata data za kibinafsi na data za kifedha za walipa ushuru. #MulikoLaKaya

Rais William Ruto amesema kupitia mfumo mpya wa kufadhili vyuo vikuu nchini, kwa sasa kuna rasilimali za kutosha zinazoelekezwa katika vyuo vikuu nchini. #MulikoLakaya

Rais William Ruto amesema kupitia mfumo mpya wa kufadhili vyuo vikuu nchini, kwa sasa kuna rasilimali za kutosha zinazoelekezwa katika vyuo vikuu nchini. #MulikoLakaya