Umoja wa Mataifa
@umojawamataifa
Akaunti rasmi ya Umoja wa Mataifa. Kwa amani, utu & usawa katika ulimwengu wenye ustawi.
ID: 67706757
https://news.un.org/sw/ 21-08-2009 20:15:32
34,34K Tweet
29,29K Followers
691 Following
"Kwenye lango la Amazon, mataifa yamefikia makubaliano yanayoonesha bado yanaweza kuungana kukabiliana na changamoto ambazo hakuna nchi inayoweza kuzishinda peke yake." - António Guterres akihitimisha #COP30. Zaidi: news.un.org/sw/story/2025/…
“Sasa ni wakati wa uongozi na maono.” - António Guterres kwenye #G20 Afrika Kusini. Dunia inahitaji viongozi wanaoweza kutumia ushawishi wao kusukuma amani, uwakilishi wenye usawa, na hatua madhubuti za kiuchumi na za tabianchi. news.un.org/sw/story/2025/…
Wengi wanajua mifuko, chupa, na mirija ina plastiki, lakini vifaa vingi vingine vya kila siku pia vina plastiki. UN Development imebaini vitu 10 vinavyotumiwa kila siku ambavyo vina plastiki nyingi, lakini hatugundui: stories.undp.org/hiding-in-plai… #BeatPlasticPollution
“Kwa wale wote walioandamana, kujadiliana, kushauri, kuripoti na kuhamasisha, msikate tamaa. Historia iko upande wenu, na #UN uko nanyi.” Baada ya #COP30 kumalizika #Brazil, António Guterres ameahidi kuendelea kusukuma mbele uwajibikaji wa tabianchi. bit.ly/4oYvvtL
Mawaziri na viongozi kutoka nchi 44 maskini zaidi duniani wameaahidi kuharakisha ujenzi wa viwanda jumuishi na kuimarisha uthabiti mbele ya changamoto za kimataifa, katika mkutano wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa uliofanyika #Riyadh. UNESCO 🏛️ #Education #Sciences #Culture 🇺🇳 news.un.org/sw/story/2025/…
“Lazima tuchague heshima ya binadamu na haki za binadamu.” - António Guterres kwa viongozi wa dunia hivi karibuni akisisitiza kwamba kulinda haki za binadamu ni muhimu ili watu waishi kwa amani na ustawi. “Haki za binadamu si mapambo ya amani, ni msingi wake wa kweli.
Kuomba hifadhi ni haki ya msingi ya binadamu kwa watu wanaokimbia vurugu, mateso, vita au majanga. Kila mtu ana haki ya kutafuta hifadhi. UNHCR, the UN Refugee Agency inafanya kazi duniani kote kusaidia watu waliolazimika kukimbia makwao.
Zaidi ya maafisa 5,600 wa jeshi na polisi kutoka #Bangladesh wanatoa huduma kwa ajili ya amani katika misheni saba za UN Peacekeeping duniani, wakiwaacha familia zao ili kuwalinda walio hatarini zaidi. Tunawashukuru wanawake na wanaume hawa jasiri kwa huduma na kujitolea kwao.
Mchakato wa kumchagua Katibu Mkuu mpya wa #UmojawaMataifa umeanza rasmi. "Uteuzi huu utakuwa ujumbe wenye nguvu kuhusu sisi ni nani na kama kwa kweli tunawatumikia watu wote wa dunia, ambao nusu yao ni wanawake na wasichana." - Annalena Baerbock Fahamu zaidi: un.org/pga/80/2025/11…
“Kwa wale wote walioandamana, kujadiliana, kushauri, kuripoti na kuhamasisha, msikate tamaa. Historia iko upande wenu, na #UmojaWaMataifa uko pamoja nanyi.” - António Guterres akiahidi kuendelea kusukuma mbele uwajibikaji wa hali ya hewa na mshikamano wa kimataifa.
Uongo unaua. Ukweli unaokoa maisha. Tunahitaji ukweli kuliko wakati wowote ule. Tunahitaji uandishi wa habari huru kuliko wakati wowote ule. Onesha mshikamano wako na vyombo vya habari. #PressFreedom UNESCO 🏛️ #Education #Sciences #Culture 🇺🇳