Presidential Delivery Bureau (PDB) - Zanzibar (@pdbzanzibar) 's Twitter Profile
Presidential Delivery Bureau (PDB) - Zanzibar

@pdbzanzibar

PDB is an institution under President's Office - State House aiming in coordinating, accelerating and following up the delivery of the key priority projects.

ID: 1599763754056572928

linkhttp://www.ikuluzanzibar.go.tz calendar_today05-12-2022 13:53:32

1,1K Tweet

991 Followers

520 Following

Presidential Delivery Bureau (PDB) - Zanzibar (@pdbzanzibar) 's Twitter Profile Photo

1/3: Taasisi ya ZPDB ikiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Profesa Mohammed Hafidh Khalfan wake ilipokea ugeni mkubwa wa Rais wa taasisi ya TIKA (Turkish Cooperation and Coordinator Agency), Bwana Serkan Kayalar kutoka nchini Uturuki.

2/3: Ugeni leo umetembelea Ofisi za ZPDB, Ikulu kwa Mhe. Rais, Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar na kisha Chuo Cha Kiislamu kilichopo Mazizini. Katika maeneo ya ushirikiano yaliyozungumzwa ni Elimu, Sanaa ya Uandishi (Caligraphy), Utunzaji wa Nyaraka, Utalii hasa Halal Tourism nk.

3/3: Rais huyo wa TIKA amefurahishwa na maendeleo ya Zanzibar yanayopigwa kwa kasi na Serikali na alisema taasisi yake imekubali na ina kila sababu ya kuiunga mkono Zanzibar katika safari yake kubwa ya maendeleo na mafanikio katika sekta mbalimbali.

1/2: Taasisi ya ZPDB ilishuhudia utiaji saini wa Hati ya Maelewano (MoU) Kati ya Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Taasisi ya Commonwealth of Learning ya Canada kwa lengo la kuwawezesha vijana wa Zanzibar kupata ujuzi wa kazi na ajira mbalimbali ndani ya nchi na nje.

2/2: Utiaji saini huo ulihudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ndugu Khamis Abdullah, Makamu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar, Mkuu wa Chuo cha Teknolojia cha Karume, Makamu Mkuu wa Chuo cha Zanzibar, Kamishna wa Kazi Zanzibar na kadhalika.

Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar atembelea Ofisi za ZPDB kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na ZPDB. Mkurugenzi huyo alikutana na Mtendaji Mkuu wa ZPDB ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar.

Taasisi ya ZPDB kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania (OUT) iliendesha na kukamilisha Mafunzo maalum ya kuhusu Misingi ya Ufuatiliaji na Usimamizi wa Miradib kwa Watendaji wa Serikali. Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa ZURA, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

Hongera kwa Watanzania wote. Tuendelee kudumisha amani, utulivu, umoja na mshikamano. Muungano ni dhamana, heshima yetu, nguzo yetu na tunu ya Taifa letu.

1/2: Taasisi ya ZPDB iliungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Viongozi wa; Kitaifa, dini na wengineo pamoja na ndugu, jamaa na marafiki katika kushiriki mazishi ya aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali Charles Martin Hilary

2/2: Mwili wa Bwana Charles Martin Hilary uliagwa katika viwanja vya Kisonge Zanzibar ambapo Mkurugenzi huyo aliongoza Idara ya Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar. Ujumbe wa ZPDB uliongozwa na Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wake, Dkt. Josephine Rogate Kimaro. Buriani Charles Hilary.