suleiman yeri
@suleimanyeri
Journalist, News Anchor @ktnnewske Liverpool FC @LFC die hard. Views are my own.
ID: 264693242
https://www.tiktok.com/@suleimanyeri?_t=8iivbyTF9cn&_r=1 12-03-2011 09:14:20
5,5K Tweet
7,7K Followers
1,1K Following
Ritimo Vitalys: Kwangu, yule aliyerusha kile kiatu, lengo la kukirusha nidio la maana kuliko kiatu chenyewe. #Yanayojiri suleiman yeri
Huku mgomo wa madaktari ukiendelea katika kaunti kadhaa humu nchini, muungano wa wauguzi umetishia kujiunga nao katika mgomo ili kuwajibisha serikali kutatua changamoto zinazowakumba nyanjani. #Yanayojiri suleiman yeri
Aliyekuwa gavana wa Meru Kawira Mwangaza apambana na polisi waliokuwa wakimzuia kuendesha mkutano katika soko la Igoji, eneobunge la Imenti Kusini. #Yanayojiri suleiman yeri
Wizara ya Maendeleo ya Kijamii ya Mandera yajiungua na ulimwengu kusherekea siku ya kimataifa ya kina mama kwa kuwazawidi kina mama waliojifungua katika hospitali ya rufaa ya Mandera. #Yanayojiri suleiman yeri
Mwakilishi wa wanawake wa Nairobi Esther Passaris ajumuika na wanawake wa mtaa wa shauri moyo kuadhimisha siku ya kina mama. #Yanayojiri suleiman yeri
Mbunge wa Embakasi Kaskazini, James Gakuya atoa shinikizo kwa Naibu Rais Kithure Kindiki kujiuzulu akisema hakuingia ofisini kihalali. #Yanayojiri suleiman yeri
Wito watolewa kwa jamii inayoishi na changamoto ya ulemavu katika Kaunti ya Kisumu kujisajili kwenye shirika linalosimamia maswala ya walemavu humu nchini. #Yanayojiri suleiman yeri
Wavuvi kutoka kaunti ya Kilifi wadai kwamba uhaba wa samaki unaoshuhudiwa sasa unatokana na matumizi mabaya na utupaji ovyo wa taka za plastiki katika bahari ya Hindi. #Yanayojiri suleiman yeri
Zaidi ya nafasi elfu kumi za ajira zimebuniwa katika Kaunti ya Kilifi kupitia juhudi za serikali ya kaunti hiyo za kufufua sekta ya utalii. #Yanayojiri suleiman yeri
Ghasia zashuhudiwa nyumbani kwa George Natembeya baada ya maafisa wa EACC kufanya oparesheni nyumbani kwake Kitale leo asubuhi. #MbiuYaKTN suleiman yeri
Mkutano wa aliyekuwa Gavana wa Meru Kawira Mwangaza watibuliwa, maafisa wawatawanya waliohudhuria. #MbiuYaKTN suleiman yeri
Wakazi wa mitaa ya Dandora, Kayole na Soweto jijini Nairobi wanufaika na kambi ya matibabu ya bure. #MbiuYaKTN suleiman yeri
Mwanasheria mkuu Dorcas Oduor akanusha madai kuwa muhuri rasmi wa serikali umehamishwa. #KTNLeo suleiman yeri
Rais Ruto na Raila waanza ziara eneo la Nyanza. #KTNLeo suleiman yeri
Wakenya waendelea kumwomboleza Ngugi Wa Thiong'o. #KTNLeo suleiman yeri
Wakazi wa Nakuru waishi na hofu baada ya kuongezeka kwa visa vya uhalifu #KTNLeo suleiman yeri
Wataalamu wa teknolojia wahoji kuwa teknolojia ya Akili-Unde(AI) yatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika mageuzi ya utendakazi barani Afrika. #KTNLeo suleiman yeri