
Holy
@yose_hoza
Digital Inclusion | Telecommunication Engineer
ID: 3039495909
15-02-2015 19:26:56
433,433K Tweet
160,160K Followers
32,32K Following


Je, unajua kuwa Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania Toleo la 2024 imeweka vijana katikati ya ajenda ya diplomasia? Kutoka ajira hadi ushiriki wa kimataifa, fursa zimejaa! Twende pamoja kupitia jukwaa la #ElimikaWikiendi kufahamu kwa undani zaidi MFA Tanzania mahmoud Kombo


Sera ya Mambo ya Nje 2024 inatutambua vijana kama nguzo muhimu ya uchumi wa kidiplomasia, tukichangia zaidi ya 60% ya nguvu kazi ya taifa. #ElimikaWikiendi MFA Tanzania mahmoud Kombo

Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania 2024 inalenga kuongeza uwakilishi wa vijana katika taasisi za kimataifa na kuimarisha ushiriki wetu katika masuala ya kidiplomasia. MFA Tanzania mahmoud Kombo #ElimikaWikiendi

Sera mpya ya Mambo ya Nje 2024 inasisitiza umuhimu wa vijana kujihusisha na ujasiriamali wa kimataifa ili kukuza diplomasia ya uchumi. MFA Tanzania #ElimikaWikiendi

Kupitia Sera hii, Vijana tunahimizwa kutumia majukwaa ya kimataifa kuwasilisha sauti zetu, kuonesha ujuzi lakini zaidi kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia majukwaa hayo. #ElimikaWikiendi MFA Tanzania

Sera mpya inahimiza vijana wa diaspora na waishio nje ya nchi kuwekeza nyumbani kwa kushirikiana na wadau wa kimataifa. mahmoud Kombo MFA Tanzania #ElimikaWikiendi

Sera inasisitiza umuhimu wa ujasiriamali wa vijana kwa kuuza bidhaa za Tanzania kwenye masoko ya SADC, EAC na nchi nyingine nje na ndani ya Afrika. MFA Tanzania mahmoud Kombo #ElimikaWikiendi

Tanzania kupitia sera hii, ina mpango wa kuendelea kukuza Kiswahili kimataifa, ikitumia vijana kama walimu, wasanii, na wanadiplomasia wa lugha. mahmoud Kombo MFA Tanzania #ElimikaWikiendi

Serikali inalenga kuandaa vijana kushiriki kwenye medani za amani na usalama kimataifa kupitia mafunzo ya kidiplomasia. MFA Tanzania mahmoud Kombo #ElimikaWikiendi

Vijana tunahimizwa kujiunga na mashirika ya kimataifa kupitia nafasi za mafunzo, ubalozi wa wanafunzi, na fellowship za kimataifa. MFA Tanzania mahmoud Kombo #ElimikaWikiendi

Sera hii inaendelea kuchochea fursa za vijana kushiriki ktk mipango na mikutano mbalimbali ya kimataifa, ikiwemo midahalo kuhusu mabadiliko ya tabianchi kupitia mikataba ya kimataifa kama UNFCCC na Mkataba wa Vijana wa Umoja wa Afrika #ElimikaWikiendi mahmoud Kombo MFA Tanzania

Mapungufu ya Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania 2024 (kwa mujibu wa uchambuzi wangu binafsi) ni haya yafuatayo: (Tweet inayofuata) #ElimikaWikiendi MFA Tanzania mahmoud Kombo

1. Ingawa sera inataja vijana kama kundi muhimu, haijaweka mkakati mahsusi ya utekelezaji kwa vijana katika nyanja za diplomasia, biashara ya kimataifa, au uwakilishi wa kimataifa. Inabaki kuwa katika lugha ya jumla #ElimikaWikiendi MFA Tanzania mahmoud Kombo

2. Sera inatumia maneno kama "kushirikisha vijana zaidi", "kukuza ubunifu", lakini hakuna viashiria vya kupima mafanikio (KPIs) au muda wa utekelezaji wa hatua hizo. MFA Tanzania mahmoud Kombo #ElimikaWikiendi

3. Pamoja na Tanzania kuwa mwanachama wa ICGLR, AU na UN, sera haijaweka wazi nafasi ya vijana katika ujenzi wa amani, mapambano dhidi ya itikadi kali, na usuluhishi wa migogoro. mahmoud Kombo MFA Tanzania #ElimikaWikiendi

Nashauri Wizara iandae mkakati wa kuweka viashiria mahsusi vya kupima ushiriki wa vijana (Youth KPI's) katika utekelezaji wa sera ya mambo ya nje, kwa uwazi na uwajibikaji. mahmoud Kombo MFA Tanzania


