
CHADEMA Tanzania
@chadematz
The Main Opposition Political Party in Tanzania ✌🏼
ID: 3309230189
https://whatsapp.com/channel/0029VaCuWWsEgGfGYYqUaS3X 05-06-2015 12:52:05
24,24K Tweet
793,793K Followers
13 Following


Makamu Mwenyekiti Bara Tundu Antiphas Lissu akiongoza maandamano ya amani Mkoa wa Iringa youtube.com/live/l45C244E2…

Makamu Mwenyekiti Bara Tundu Antiphas Lissu akiongoza maandamano ya amani Mkoa wa Iringa





"Tunajiuliza Taifa la Tanganyika lipo wapi?. CCM wanatung`ang`ania kwenye muungano ambao hauna ridhaa ya wananchi. Watanzania wanapenda muungano, hatuwachukii wenzetu wa Zanzibar ila na sisi tunataka tuwe na Serikali ya Tanganyika." Mhe. Freeman Mbowe

"Tupo wananchi milioni 64 leo, tunatawaliwa na visiwa vya Zanzibar. Zanzibar wanajitawala wana Rias wao, wanatukopesha na sisi Rais wetu . Yaani tunatawaliwa na Rais wa nchi jirani. Zanzibar ni nchi na wana haki yao, tunataka watanzania muamke." Mhe. Freeman Mbowe

"Tunataka muungano wenye haki kwa pande zote mbili, kama wana haki ya kuwa na Serkali yao na sisi tuwe na haki ya kuwa na serikali yetu kisha tuwe na Serikali ya muungano kwa yale mambo machache ambayo tunashirikiana." Mhe. Freeman Mbowe

"Yale yaliyofanyika 2020 na 2019 mpaka leo yanafanyika. Vyombo vyote na wadau wote, taasisi za dini wameshauri Serikali haisikii." Mhe. Freeman Mbowe


"Tunakwenda kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa miezi minne ijayo, hatujui kanuni, sisi ni wachezaji. Wanaojua ni Serikali na CCM, wanahodhi michakato yote." Mhe. Freeman Mbowe

"Watu wana hasira kuliko mnavyofikiria, epusheni taifa hili na athari hizo. Hii nchi ni kama imemwagiwa mafuta, itachukua kichaa mmoja tu kuchukua njiti ya kiberiti akawasha na nchi ikalipuka. Ikifikia hatua hiyo ni ngumu kuiendesha nchi." Mhe. Freeman Mbowe

"Hivi vitimaalum vya kutoa kwa kinamama wakati mwingine ni kama kuwa dhalilisha wanawake. Tukasema tuweke mfumo wa uchaguzi ambao kinamama wenyewe kwa wenyewe watachuana katika jimbo la uchaguzi. Hilo wazo zuri halijafanyiwa kazi na Serikali." Mhe. Freeman Mbowe

Makamu Mwenyekiti Bara Tundu Antiphas Lissu akipokea zawadi ya Mbuzi kutoka kwa wananchi wa Kata ya Chitemo Jimbo la Mpwapwa alipofika kufanya mkutano wa hadhara asubuhi ya leo Mei 9, 2024 na jioni anatarajia kufanya mkutano Jimbo la Kibakwe.


Makamu Mwenyekiti Bara Tundu Antiphas Lissu akiteta jambo na Mwenyekiti wa Wilaya ya Mpwapwa Ezekiel Chisinjira wakati alipofika katika Kijiji cha Chunyu Wilaya ya Mpwapwa.


Makamu Mwenyekiti Bara Tundu Antiphas Lissu alivyofika Police Force TZ Mkoa wa Dodoma kukabidhiwa gari lake ambalo lilikuwa chini ya Police Force TZ kama kielelezo kufatia tukio la kupigwa na watu wasiojulikana Spet 7,2017 na leo Meyi 17,2024 amekabidhiwa gari hilo bila kupatiwa taarifa ya uchunguzi

Tumewasilisha maoni Tume ya Uchaguzi juu ya kanuni za kuboresha daftari la Kudumu la Wapiga kura! Tunaitaka Tume izingatie kwani Kwa kanuni zilivyo hatuoni nia njema ya uandikishaji wa Haki wa wapiga kura nchini ili kufikia uchaguzi Huru na haki Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi CHADEMA TANZANIA